Tuesday, November 29, 2011

3) KANISA LA PERGAMO(Ufunuo 2:12-17)

12)Na kwa malaika lililoko Pergamo andika;
       Haya ndiyo ananenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili. Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, walahukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuwawa kati yenu, hapo akaapo Shetani (14) Lakini ndiyo maneno machache washikao mafundisho ya Balaanu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini. (15)Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vilevile (16) Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upaga wa kinywa changu. (17) Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea


Kanisa la Pergamo
  • Neno Pergamo humaanisha 'Kimo au Mwinuko'
  • Mji wao wa kwanza ulijengwa juu ya kilima chenye mawe mengi kilichoinuka futi elfu moja
  • Kanisa hili lilidumu kati ya miaka ya 313 B.K-538B.K
  • Hapa ni kwamba mateso yote yalikoma
  • Hapa ndipo mfalme Constantine (Konstantino) mwenyewe alijifanya Mkristo, kumbe kanisa lilikuwa katika hatari kubwa ! Kumbe ile ''Siri ya Uasi'' ilipoanzia. Yeye ndiye aliyebadilisha wakati, saa na majira.(alitimiza unabii wa Danieli 7:25)
Sanamu la Constatine
  • Kiti cha enzi cha Shetani humaanisha- mahali anapofanyia kazi, ndipo alipofanya kazi kubwa kwa kutumia Conctatine na kuleta anguko kubwa mpaka leo.

  • Historia haitufahamishi mtu yeyote aliyeitwa 'Antipa', lakini inaelekeza ni kikundi cha watu waliopoteza maisha yao kwa sababu ya upapa(papacy), 'Anti' humaanisha kupinga na 'pa' maana yake ni baba au Papa(pope)

  • Wengine walikana imani yao ili kufainika na utajiri na heshima za kibinadamu au ulimwengu kama vile Baalamu alivyokuwa tayari kuwalaani na kupewa tuzo la thamani (Hesabu 22-25)

  • Biblia ilifika hadi Ikulu za wafalme nao wakaitafsiri vibaya.

  • No comments:

    Post a Comment