Tuesday, November 29, 2011

2) KANISA LA SMIRNA(Ufunuo 2:8-11)

(8) Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika;
       Haya ndiyo annenayo yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai. (9) Naijua dhiki yako na umaski wako,(lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi bali ni sinagogi la Shetani. (10) Usiogope mambo yatakayokupata; tazama huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa, taji ya uzima. (11) Yeye aliye na sikio, na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili

KANISA LA SMIRNA
  • Neno Smirna humaanisha kitu kinachoonukia vizuri
  • Kanisa hili lilikuwepo kati ya muda au miaka wa mateso na maumivi ambacho kilikuwa miaka ya 100 B.K mpaka 313 B.K
Mungu hafurahii kuona watu wake wakiteswa, lakini uaminifu na utii wao katika majaribu ulimfurahisha na kuliinua jina la Mwokozi aliyewafia

Mungu anawaambia kanisa la Smirna kwamba anawajua wale wanaosema kwamba wenyewe ni Wayahudi lakini si Wayahudi, Basi hao Wayahudi ni nani?

Wayahudi ni wale watu ambao walipewa kwa sana neno la Mungu na kulikataa, ndipo Mungu akaamua kuwapa mataifa katika mwaka wa 33B.K(hili nalo ni somo)

Lakini kadhalika kulikuwa na Wayahudi fulani ambao walikuwa wanashika neno la Mungu, lakini mtume Paulo anasemaje kuhusu kuwa myahudi kwa uhakikia (Warumi 2:28,29) unasema 'uyahudi wa mtu hauonekani kwa nje bali kwa ndani ambaye sifa yake haitoki kwa mwanadamu bali hutoka kwa Mungu'

Basi katika wakati ule watu walijidai kumfuata Kristo, lakini katika mioyo yao wakipenda ulimwengu na ubunafsi, lakini kwa wao walilishika neno la Mungu walitaabishwa na kuanza kufuata nyao, desturi na Imani ya Kristo

SANAMU LA MFALME DIOCLETIAN
Sasa, maana ya siku kumi ni nini?
Ni siku za mateso, ni kipindi katika muda wa unabii, siku moja husimama badala ya mwaka mmoja(Tazama Hesabu 14:34; Ezekiel 4:6)
    Kilikuwa ni kipindi ambacho kilikuwepo ndani ya wakati wa kanisa la Smirna (100 B.K-313B.K) ambapo, utawala wa mfalme huyu katili ambaye alikuwa anawatesa watu wa Mungu Utawala wa Mfalme Diocletian, (ambaye anafananishwa na sinagogi la shetani)

Lakini kumbuka wale watu waliokufa katika Imani hawana cha kuogopa ndio maana Yohana anawatia moyo.



                                                                                               
                                                                                                           

No comments:

Post a Comment