1) KANISA LA EFESO (Ufunuo:2:2-7)
2)Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume na sio, ukawaona waongo; (3) tena ulikuwa na subira haukuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka (4)lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza (5)basi, kumbukuka ni wapi ulipoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza, Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu (6) Lakini unalo neon hili, kwamba wachukia matendo ya wanikolai, ambayo na mimi nayachukia. (7) Yeye aliye na sikio, na asikie, neon hili ambalo roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa kula matunda ya mti wa uzima, uliyo katika bustani ya Mungu.
· Efeso humaanisha tamanio
· Kanisa la Efeso lilikuwa ni taa ing’aayo katika giza tororo,lilikuwa likifaulu kila sehemu na watu wenye tamaa,viburi walibadilika.
· Lakini kidogo kidogo badadiliko yalianza kuingia na wengi walipoteza imani yao ile ya kwanza, Je ni nani aliyewapoteza?
· Katika mstari wa sita ,Mungu anasema anawachukia wanikolai, Basi wanikolai ni akina nani?
· Katika Matendo6:5 tunaona kuna mashemasi saba walichaguliwa kuwahudumia wajane kwani walikuwa wanasahulika ndimo kulikuwa na Stefano, Filipo vilevile palikuwepo na Nikolao, pakawa na kikundi cha wanikolao ambao walihubiri habari potofu za Mungu.
· Basi Yohana akaongozwa na roho mtakatifu kuliandikia kanisa la Efeso akiwapa maonyo kutowasikiliza hao,
Lakini walipewa chaguo,“yeye aliye na sikio, na asikie neon hili ambalo roho anayaambia makanisa.Yeye ashinaye nitampa kula matunda ya mti wa uzima,ulio katika bustani ya Mungu”